Saturday, June 26, 2021

Chapati za kumi Nairobi


 CHAPATI ZA KUMI NAIROBI

    Nairobi, mji mkuu nchini Kenya wenye watu takriban milioni 4.397 ambao asili mia 60% ya wakaazi hao ni wafanya biashara. Uuzaji wa chapati Nairobi umekuwa ukinawiri kifaida ndani na nnje ya mji, ila kinachowapa  taabu wanunuzi ni ambapo chapati hizi zinapouuzwa bei ghali kinyume na matarajio yao.

                  Kutokana na utafiti wa matumizi ya ngano, imebainika wazi kwamba katika kila mwaka ngano hutumika kwa asii mia 47% ikilinganishwa na vyakula vyengine hata kwa jinsi bei ya vyakula vya ngano kama chapati kuuzwa bei ghali. 

                   Wanunuzi wengi wa chapati huwa vijana wanaofanya vibarua na wanabiashara wadogowadogo katika masoko na vituo vya mabasi, mara nyingi wateja wa chapati hupewa chakula hiki pamoja na mchuzi wa bure katika vibanda na hoteli nyingi zilizopo kando kando ya barabara na pia nnje ya maduka makbwa makubwa mjini Nairobi, 


                 Iwapo mtu angetaka chapti za shilingi kumi basi ni vyema kuwa tayari kuingia katika soko kubwa mjini  Nairobi, 'Muthurwa'. Katika soko hili chapati huuzwa kwa shilingi kumi, ni wachache wanaojua mahali ambapo chapati hizi za shiliingi kumi huuzwa. Julai 20.2021 niliweza kufika katika kibanda kimoja Muthurwa na kununua chapati ya shilingi kumi, hapa nilipakuliwa chapti hio kwa mchuzi wa maharagwe ambao uikuwa mchuzi wa bure. ''Hoteli hii hupata watu wasiopungua mia mbili kila siku'' alisema meneja wa hoteli hio. Kizuri zaidi katika hoteli hii ni kwamba mteja anaweza kulipa kupitia simu kwa mtandao wowoe ule.

            Magharibi mwa soko hili la Mudhurwa ndipo hoteli kama hii ya chapati za shilingi kumi na vyakula vyengine vitamu vya bei ya chini hupatikana. Mara kwa mara upande huu wa soko hupaswi kuamini watu hususan kwa barabara. Ni vizuri kuwa na ufahamu kamili wa pale unapoelekea katika soko hili maana vijana waliokaa kandokando ya njia hizi huwa na njama za kuwapora wapita njia pasi kutaka kujua wakati au masaa ya siku .

                 

Friday, June 25, 2021

ZINZI



 ZINZI


                  

Mara hii alirudi nyumbani akiwa mwenye huzuni, ‘’ wamekuchokoza tena?’’ aliuza bibi yake, Zinzi kwa unyonge akamkumbatia bibi yake anaemuona kama mama na baba katika maisha yake, mschana asiye na ugomvi akajiachilia kifuani mwa bibiye huku machozi yakimtoka kwa uchungu, kwa kigugumizi akajibu ‘’ndi-ndi-o bi-bi’. Zinzi mwenye umri wa miaka minane alikuwa amekerwa na kuchoka  na tabia za waschana wa shule ya mwembeni.

               Mschana kama zinzi wa darasa la nne hangeweza kujitetea anaposumbuliwa kwa maswali ya kejeli na wanafunzi waliomzidi umri na darasa, kwa hivyo alikuwa akinyamaza kama maji ya mtungini vijana wale walipokuwa wakimuuliza maswali kuhusiana na atokapo, iwapo amebeba vitabu au mawe begini na maswali mengine mengi ya kukera.

             Siku moja zinzi akiwa nyumbani, bibi yake alimuita na kumfunza kupiga mluzi kama firimbi ili kupata usaidizi kutokana na wale wanaomchokoza shuleni. Zinzi siku hiyo hakujuwa ni msaada gani atakaopata ila aliamua tu kumuamini bibi yake. 

             Ikatokea siku, zinzi akakutana na wanafunzi watano waliokuwa na sare chafu zilizojawa vumbi na viraka, ‘’mbona leo hujatubebea soda?’’ mmoja wao alimuuliza Zinzi,  kabla mwengine kufungua mdomo, Zinzi akapiga mluzi kwa nguvu, kukatokea njiwa wengi angani wakawanyeshea matone ya mavi na uchafu mwingi wanafunzi waliokuwa wakimchokoza Zinzi. Siku hiyo wanafunzi wale walipata aibu na kuchekelewa na wanafunzi wengine wote waliokuwa barabarani, zinzi alifurahi sana maana tangu siku hiyo wanafunzi wale wanapomuona humpisha na kunyamaza wasimuulize hata salamu. 

               

BINTI YETU

BINTI YETU Ni heri basi arudi, kuliko kututesea, Kwa sasa hatuna budi, sisi kama familia, Hizo dhiki zimezidi, mrudishe twakwambia, Binti ye...