Friday, June 25, 2021

ZINZI



 ZINZI


                  

Mara hii alirudi nyumbani akiwa mwenye huzuni, ‘’ wamekuchokoza tena?’’ aliuza bibi yake, Zinzi kwa unyonge akamkumbatia bibi yake anaemuona kama mama na baba katika maisha yake, mschana asiye na ugomvi akajiachilia kifuani mwa bibiye huku machozi yakimtoka kwa uchungu, kwa kigugumizi akajibu ‘’ndi-ndi-o bi-bi’. Zinzi mwenye umri wa miaka minane alikuwa amekerwa na kuchoka  na tabia za waschana wa shule ya mwembeni.

               Mschana kama zinzi wa darasa la nne hangeweza kujitetea anaposumbuliwa kwa maswali ya kejeli na wanafunzi waliomzidi umri na darasa, kwa hivyo alikuwa akinyamaza kama maji ya mtungini vijana wale walipokuwa wakimuuliza maswali kuhusiana na atokapo, iwapo amebeba vitabu au mawe begini na maswali mengine mengi ya kukera.

             Siku moja zinzi akiwa nyumbani, bibi yake alimuita na kumfunza kupiga mluzi kama firimbi ili kupata usaidizi kutokana na wale wanaomchokoza shuleni. Zinzi siku hiyo hakujuwa ni msaada gani atakaopata ila aliamua tu kumuamini bibi yake. 

             Ikatokea siku, zinzi akakutana na wanafunzi watano waliokuwa na sare chafu zilizojawa vumbi na viraka, ‘’mbona leo hujatubebea soda?’’ mmoja wao alimuuliza Zinzi,  kabla mwengine kufungua mdomo, Zinzi akapiga mluzi kwa nguvu, kukatokea njiwa wengi angani wakawanyeshea matone ya mavi na uchafu mwingi wanafunzi waliokuwa wakimchokoza Zinzi. Siku hiyo wanafunzi wale walipata aibu na kuchekelewa na wanafunzi wengine wote waliokuwa barabarani, zinzi alifurahi sana maana tangu siku hiyo wanafunzi wale wanapomuona humpisha na kunyamaza wasimuulize hata salamu. 

               

BINTI YETU

BINTI YETU Ni heri basi arudi, kuliko kututesea, Kwa sasa hatuna budi, sisi kama familia, Hizo dhiki zimezidi, mrudishe twakwambia, Binti ye...